Home – SDGs for All

A project of the Non-profit International Press Syndicate Group with IDN as the Flagship Agency in partnership with Soka Gakkai International in consultative status with ECOSOC

Watch out for our new project website https://sdgs-for-all.net

Mradi wa Kihistoria Unakusudia Upanzi wa Miti nchini Togo – Fursa za Mapato kwa Wanawake

Na Ramesh Jaura

BERLIN | TOKYO (IDN) – Togo iliyoko Afrika Magharibi ni mahali pa mradi wa hatua muhimu kati ya Soka Gakkai, shirika la jamii ya kimataifa ya Wabudha na Shirika la Kimataifa la Mbao za Kitropiki (ITTO). Mashirika hayo mawili yametia saini memoranda ya kuzindua mradi wa upanzi wa miti unaotoa fursa za mapato kwa vikundi vya wanawake katika maeneo mawili ya vijijini nchini Togo.

Memoranda inayohusisha mchango wa yen milioni 10 (Dola za Marekani 93,300) kwa awamu ya kwanza ya mwaka mmoja ya mradi huo ilisainiwa mnamo Julai tarehe 1 katika makao makuu ya Soka Gakkai (SG) huko Tokyo. Mradi utaanza Septemba tarehe 1.

Read More...

Wakenya Ni Wabunifu katika Kupata Njia za Kupambana na COVID-19

Na Justus Wanzala

BUSIA, Kenya (IDN) – Ni mchana wenye joto katika kituo cha mabasi katika kituo cha soko cha Mungatsi, Kaunti ndogo ya Nambale, katika Kaunti ya Busia, Magharibi mwa Kenya. Watu wengi, idadi kubwa yao wasafiri wanapanga foleni kuosha mikono yao. Kila mtu anadumisha umbali kutoka kwa mwingine wakati wanaosha mikono yao na kuabiri magari ya huduma za umma wakielekea maeneo yao mbalimbali.

Read More...

Athari ya COVID-19 Inakumba Afrika – Video Iliyohuishwa Inawaambia Watoto Kuihusu

Na Lisa Vives, Mtandao wa Taarifa wa Kimataifa

NEW YORK (IDN) – Wakati Afrika, kama jamii ya kimataifa kwa ujumla, inashiriki katika vita vikali dhidi ya virusi vya korona, mtaalamu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ameuliza kuhusu makadirio ya kutisha ya wale walioathiriwa na COVID-19. Wakati huo huo, Ghana kwa hatua ya mshangao imeamuru kuondolewa kwa kusitishwa kwa shughuli za kawaida kwa kiasi fulani. Kirusi kilichoenea sana kinaingiza Rwanda katika ‘mikopo’ mikubwa chini ya upunguzaji wa deni.

Read More...

Idadi ya Watu Duniani Inatarajiwa Kufika Karibu Bilioni 10 ifikapo mwaka wa 2050

Na Jaya Ramachandran

NEW YORK (IDN) – Ikilinganishwa na bilioni 7.7 leo, karibu watu bilioni 8.5 wanatarajiwa kukaa katika sayari ya Dunia kwa muda mfupi zaidi ya miaka kumi, na karibu bilioni 10 ifikapo mwaka wa 2050, na nchi chache tu zenye ongezeko kubwa, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa.

Matarajio ya Idadi ya Watu 2019: Mambo muhimu, yaliyochapishwa na Idara ya Idadi ya Watu wa Idara ya Umoja wa Mataifa ya Mambo ya Uchumi na Kijamii (UN DESA), yanatoa maelezo ya kina ya mifumo ya kimataifa ya idadi ya watu na matarajio. Utafiti unahitimisha kwamba idadi ya watu duniani inaweza kufikia kilele chake ikikaribia mwisho wa karne ya sasa, kwa kiwango cha karibu bilioni 11.

Read More...

Serikali za Kiafrika Zinajiunga na Wanaharakati Kupambana na Ulipizaji/Ufisadi wa Kingono

Na Kizito Makoye

DAR ES SALAAM (IDN) – Bango lenye ujumbe “Hitimu na ‘A’ sio na UKIMWI” katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, linaeleza hadithi mbaya ya wanafunzi wa kike ambao hushiriki ngono ili kupata alama za juu.

“Mwalimu wangu alitaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mimi. Nilipokataa matakwa yake ya ngono, alilipiza kisasi kwa kunipa alama za chini,” anasema Helena (si jina lake halisi).

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 anayesomea sheria, ambaye amepitia utendaji duni katika masomo yake, anazidi kuwa na wasiwasi kuhusu hatma yake ya kitaaluma.

Read More...

Wahandisi wa Nishati ya Jua wa Kike Wanatoa Mwangaza katika Vijiji vya Mbali kule Zanzibar

Na Kizito Makoye

KENDWA, Tanzania (IDN) – Giza linapoingia, Natasha Mahmood na kaka yake hupiga gumzo karibu na mwali wa taa ya mafuta taa, wakiharakisha kumaliza kazi yao ya ziada kabla mama yao aizime taa ili kuhifadhi mafuta.

“Mimi mara nyingi hujaribu kuikamilisha mapema. Lakini hilo sio suala wakati wote. Mwalimu wangu wakati mwingine huniadhibu kwa ajili ya kushindwa kukamilisha kazi yangu,” anasema Mahmood, moshi kutoka kwenye taa unapofuka ndani ya paa la mabati lililochafuliwa na masizi yanayotokana na moshi.

Read More...

Kimbunga Kilisambaratisha Afrika ya Kusini Inakabiliwa Na Changamoto Ngumu

Na Jeffrey Moyo

CHIMANIMANI, Zimbabwe (IDN) – Kimbunga kitaathiri eneo kwa miezi ijayo baada ya kuathiri njia muhimu za kupata riziki za uvuvi na kilimo katika eneo la vijijini kwa kiasi kikubwa, Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ulisema kwa kutoa maelezo juu ya uharibifu uliosababishwa na Kimbunga Kenneth kilichoshambulia Msumbiji mnamo Aprili 25, karibu wiki tano baada ya Kimbunga Idai kilichoshambulia Afrika Kusini.

Kiasi cha hekta 31,000 (ekari 76,600) za mazao zilipotea katika kilele cha msimu wa mavuno. “Eneo hilo tayari limekabiliwa na uhaba wa chakula,” msemaji Herve Verhoosel alisema.

Read More...

Angola ina Mpango wa Kuunda Vifaa vya Kijeshi vya Kirusi

Na Kester Kenn Klomegah*

MOSCOW (IDN) – Nchi nyingi za Afrika zinatafuta biashara yenye faida, uwekezaji na biashara badala ya misaada ya maendeleo. Sasa Angola, kusini ya kati ya Afrika, imetangaza mipango ya kampuni kupanua biashara yake ya kitaifa kutoka kwa kununua hadi kwa uundaji kamili wa vifaa vya kijeshi vya Kirusi kwa soko la kusini mwa Afrika, na ikiwezekana maeneo mengine katika Afrika – utambuzi unaokuja wa Kusudi la 16 la Maendeleo Endelevu unaotoa wito wa amani na haki.

Read More...

Mgogoro Ndani ya Mgogoro kwa Rohingyas

Na Naimul Haq

DHAKA, Bangladeshi (IDN) – Licha ya jitihada iliyoratibiwa vizuri ya kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi wa Rohingya katika Bazar ya Cox, mji wa pwani unaopakana na Myanmar, baadhi ya changamoto kubwa bado zinahitaji uangalizi.

Utawala wa mitaa unakubali kuwa kwa wananchi wa Myanmar zaidi ya milioni moja waliohamishwa kwa lazima wanaowasili katika muda mfupi sana, kwa kweli ni vigumu kushughulikia uharibifu wa mazingira na kupanda kwa viwango vya uhalifu vinavyowakabili watu wa mitaa.

Read More...

NEWSLETTER

STRIVING

MAPTING

MAPTING

Scroll to Top