Home – SDGs for All

A project of the Non-profit International Press Syndicate Group with IDN as the Flagship Agency in partnership with Soka Gakkai International in consultative status with ECOSOC

Watch out for our new project website https://sdgs-for-all.net

Mradi wa Kihistoria Unakusudia Upanzi wa Miti nchini Togo – Fursa za Mapato kwa Wanawake

share
tweet
pin it
share
share

Na Ramesh Jaura

BERLIN | TOKYO (IDN) – Togo iliyoko Afrika Magharibi ni mahali pa mradi wa hatua muhimu kati ya Soka Gakkai, shirika la jamii ya kimataifa ya Wabudha na Shirika la Kimataifa la Mbao za Kitropiki (ITTO). Mashirika hayo mawili yametia saini memoranda ya kuzindua mradi wa upanzi wa miti unaotoa fursa za mapato kwa vikundi vya wanawake katika maeneo mawili ya vijijini nchini Togo.

Memoranda inayohusisha mchango wa yen milioni 10 (Dola za Marekani 93,300) kwa awamu ya kwanza ya mwaka mmoja ya mradi huo ilisainiwa mnamo Julai tarehe 1 katika makao makuu ya Soka Gakkai (SG) huko Tokyo. Mradi utaanza Septemba tarehe 1.

Mradi utashughulikia mabadiliko ya hali ya hewa, umasikini na maswala ya kijinsia nchini Togo, ambapo misitu inapotea haraka na umasikini unaongezeka. Janga la virusi vya korona pia limewazuia watu kurudi vijijini, na kuongeza shida kwa rasilimali za misitu.

Soka Gakkai inakuza amani, utamaduni na elimu inayolenga kuheshimu hadhi ya maisha, na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Mtazamo ni miongoni mwa mengine: juu ya ulinzi wa mazingira ya asili kupitia miradi na taasisi ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Soka ya Mafunzo ya Kimazingira na Utafiti wa Amazon, na pia kukuza ufahamu wa hitaji kubwa la kufikia SDG kupitia miradi ya vyombo vya habari kama ile iliyo na IDN, umuhimu wa Shirika lisilo la faida la Wanahabari la Kimataifa .  Soka Gakkai ina wanachama milioni 12 ulimwenguni kote, wanaochangia jumuiya kwa msingi wa falsafa ya kibinadamu ya Ubudha wa Nichiren.

ITTO ni shirika la serikali zinazoendeleza usimamizi endelevu na uhifadhi wa misitu ya kitropiki na upanuzi na umbalimbali wa biashara ya kimataifa katika mbao za kitropiki kutoka kwa misitu inayosimamiwa kiuendelevu na kuvunwa kisheria.

Mradi wa Soka Gakkai-ITTO unaambatana na mpango wa kitaifa wa Togo wa kukabiliana na hali ya hewa (NAP) na mchango wa kitaifa ulioazimiwa (NDC) chini ya UNFCCC Mkataba wa Paris wa mwaka wa 2015. Itachangia SDGs 1 (Hakuna Umasikini), 5 (Usawa wa Kijinsia), 13 (Hatua ya Hali ya Hewa), na 15 (Maisha juu ya Ardhi).

Misitu inapungua kwa kasi nchini Togo kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa idadi ya watu inayoongezeka, upanuzi wa kilimo, unyonyaji mwingi, hafla zilizokithiri za hali ya hewa, na ukosefu wa uwezo wa kiambo wa kutekeleza usimamizi endelevu wa misitu, na kusababisha athari mbaya kwa usalama wa chakula, usambazaji wa mbao na njia za kupata riziki.

Wizara ya Mazingira na Rasilimali za Misitu (MERF) ilifunua mnamo mwaka wa 2018 kwamba kiwango cha uharibifu wa misitu ya Togo ni mojawapo ya juu zaidi ulimwenguni.

Wanawake katika jamii za vijijini ni miongoni mwa walioathirika zaidi kutokana na kukosekana kwa usawa wa kijinsia. Mradi utawasaidia kuongeza ustadi wao wa kishirika, kiusimamizi na kiufundi katika uanzishaji wa bustani ya miche na matengenezo, upanzi bora wa nishati ya kuni, kilimo cha misitu, upanzi wa chakula, na uzalishaji wa bidhaa za msitu za mbao na zisizo za mbao kwa ajili ya kuuza katika masoko ya kiambo.

Rais Mtendaji wa ITTO Dk Gerhard Dieterle alisema: “Mara nyingi watu huzungumza kuhusu kulinda msitu bila kujali maisha ya watu. Mradi huu utalinda haki za wanawake, kukuza uchumi wa vijijini na usalama wa chakula na kurejesha msitu ulioharibiwa.” Huu ndio kabisa aina ya mpango wa ubunifu, wa mashinani ambao unaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa maisha ya wanawake wa vijijini na pia kulinda misitu ya kiambo, aliongeza Dk Dieterle.

Rais wa Soka Gakkai Minoru Harada alisema shirika lake lilifurahi kusaidia mradi huo, ambao utaleta faida ya kweli kwa wanawake wa vijijini na familia zao.

Kufuatilia asili za mradi wa pamoja, chanzo cha Soka Gakkai kilieleza kuwa shirika lina nia ya kusaidia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) barani Afrika – hasa kumaliza umaskini, kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake, kuhimiza hatua ya haraka ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake, na pia kulinda, kurejesha na kukuza matumizi endelevu ya viumbe hai vya ardhini, kusimamia misitu kwa uendelevu, kupambana na kuenea kwa jangwa, na kusitisha na kukomesha uharibifu wa ardhi na kusitisha hasara ya bioanuai.

Kwa mtazamo huu, Soka Gakkai kwa miaka mingi imekuwa ikijadili njia na mbinu za kutekeleza malengo manne. Baadaye, shirika lilibadilishana maoni na ITTO ambayo ina makao yake makuu huko Yokohama, mji wa bandari kusini mwa Tokyo. Iliendeleza nia katika shughuli za shirika kulenga kukuza uwezeshaji wa wanawake na kupunguza umaskini kupitia upanzi wa miti.

Soka Gakkai pia ilijifunza kuhusu Mtandao wa Wanawake wa Afrika wa Usimamizi wa Kijamii wa Misitu (REFACOF), shirika lisilo la kiserikali (NGO), mshirika wa kiambo wa ITTO. NGO ina mafanikio katika kuendeleza shughuli ambazo Soka Gakkai iliona zinastahili kuigwa katika nchi kama vile Ivory Coast na Ghana.

Soka Gakkai ilijifunza kwamba REFACOF ilikuwa inapanga shughuli mpya sawa na kujitolewa kusaidia mradi kwa pamoja. Kulingana na memoranda ya SG-ITTO, NGO ya REFACOF itasaidia vikundi vya wanawake katika wilaya mbili masikini zaidi za Togo; Blitta na Lacs.

Katika kijiji cha Pagala-gare cha Wilaya ya Blitta, urejeshwaji wa misitu na upannzi wa kuboresha vitafanyika, na katika Wilaya ya Lacs, msitu wa jamii wa kuni utaundwa kwenye kiwanja kilichotolewa na wakuu wa kijiji cha Agouegan. Katika vijiji vyote viwili, miti ya kilimo cha msitu pia itapandwa kwenye ardhi ya familia. [IDN-InDepthNews – 05 Julai 2020]

Picha: Wanawake wanatunza bustani ya miche ya jamii iliyoundwa kama sehemu ya mradi uliokamilika wa ITTO kusaidia kurudisha mazingira ya misitu nchini Togo. Hisani: ODEF

NEWSLETTER

STRIVING

MAPTING

PARTNERS

Scroll to Top