Home – SDGs for All

A project of the Non-profit International Press Syndicate Group with IDN as the Flagship Agency in partnership with Soka Gakkai International in consultative status with ECOSOC

Watch out for our new project website https://sdgs-for-all.net

Kimbunga Kilisambaratisha Afrika ya Kusini Inakabiliwa Na Changamoto Ngumu

share
tweet
pin it
share
share

Na Jeffrey Moyo

CHIMANIMANI, Zimbabwe (IDN) – Kimbunga kitaathiri eneo kwa miezi ijayo baada ya kuathiri njia muhimu za kupata riziki za uvuvi na kilimo katika eneo la vijijini kwa kiasi kikubwa, Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ulisema kwa kutoa maelezo juu ya uharibifu uliosababishwa na Kimbunga Kenneth kilichoshambulia Msumbiji mnamo Aprili 25, karibu wiki tano baada ya Kimbunga Idai kilichoshambulia Afrika Kusini.

Kiasi cha hekta 31,000 (ekari 76,600) za mazao zilipotea katika kilele cha msimu wa mavuno. “Eneo hilo tayari limekabiliwa na uhaba wa chakula,” msemaji Herve Verhoosel alisema.

Mnamo Aprili 28, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema Katibu Mkuu “alisikitishwa sana” kwa taarifa za kupoteza maisha na uharibifu nchini Msumbiji na Visiwa vya Ngazija kutokana na Kimbunga Kenneth. Aliomba jumuiya ya kimataifa “rasilimali za ziada, ambazo zinahitajika kwa kiasi kikubwa kufadhili itikio katika muda mfupi, wa kati na mrefu”.

Mapema, nchini Zimbabwe, Kimbunga Idai – kilichoshambulia nchi za Kusini mwa Afrika kama Msumbiji, Malawi na Zimbabwe usiku wa Machi 14-15, 2019 – kilichoacha Murambi mwenye umri wa miaka 57 bila shamba la kupanda mazao yake hata msimu ufuatao wa kupanda unavyokaribia. “Kwangu kimefanya uharibifu mbaya zaidi. Nilipoteza mume kwa sababu ya kimbunga. Pia nilipoteza mashamba ambayo tulikuwa tukipanda mazao yetu, ” aliambia IDN.

Nchini Malawi, wakati mgumu zaidi umeathiri wengi kama Agness Banda mwenye umri wa miaka 71. “Ni mimi tu nilibaki katika familia yangu. Nyumba yangu iliharibiwa, familia yangu yote iliangamizwa pia na kila kitu tulikuwa nacho kama familia kiliharibiwa katika kimbunga,” Banda aliambia IDN.

“Athari za mabadiliko ya hali ya hewa zimefikia viwango vya janga katika eneo letu; vimbunga kama Idai ni moja yao,” Adias Muluzi , mtaalam wa mabadiliko ya hali ya hewa wa huko Blantyre, jiji kuu la pili la Malawi, aliambia IDN.

Kwa Msumbiji, kupigana kwa bidii kushinda athari za mabadiliko ya hali ya hewa za vimbunga viwili vya chamchela, afadhali ingehitaji ushirikiano, kama Waziri wa Afya Nazira Abdula anasema: “Kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kunahitaji jitihada za pamoja kutoka sekta mbalimbali za serikali, washirika wetu na jamii kwa ujumla”.

Kwa kuungwa mkono na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNDP), Msumbiji imekuwa na maumivu ya kuunganisha kupunguza hatari ya maafa na vipengele vya kukabiliana na hali ya hewa katika sekta kama vile kilimo, elimu, afya, miundombinu na nishati.

Nchini Zimbabwe pia, UNDP na washirika wamekuwa wakitekeleza Hazina ya Ujenzi ya Ustahimilivu ya Zimbabwe, ambayo inatoa msingi wa ushahidi wa kufanya sera juu ya ustahimilivu; huimarisha uwezo wa ustahimilivu wa jamii zilizo hatarini na hutoa jibu nafuu la dharura kupitia mitandao iliyopo ya usalama na mipango mingine inayofaa.

Hata nchini Malawi, UNDP na msaada kutoka kwa Green Climate Fund, inatoa utabiri sahihi wa hali ya hewa na kuongeza mifumo ya onyo ya mapema ya jamii kwa asilimia 75 ya wilaya ili kufaidi watu milioni mbili.

Mkurugenzi wa Eneo wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa wa Afrika, Juliette Biao, pia amesisitiza haja ya uwekezaji zaidi na wa dharura katika mazingira ya msingi ya kupunguza hatari ya maafa na mabadiliko ya hali ya hewa ili kupunguza hatari ya kibinadamu na kifedha ya majanga ya asili.

“Usimamizi wa kimazingira wa sauti, athari za mabadiliko ya hali ya hewa na majibu ya maafa vinahusishwa kwa karibu na vinahitaji njia bora zaidi na ya kina ya usimamizi wa hatari ya maafa,” anasema Biao.

Joseph Tasosa, mkurugenzi wa Itibari ya Kimazingira ya Zimbabwe ana uhakika wa kuweka mkazo “haja ya kufikiria uhamasisho ulioboreshwa na mifumo ya maandalizi ya dharura ili kuimarisha ustahimilivu wa jamii za kiambo athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanayozidi”

Ndani ya muktadha wa Mfumo wa Sendai wa Kupunguza Hatari ya Maafa (2015-2030), Idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa iliendeleza Toleo la Pili la Uhamasisho na maandalizi ya dharura katika kiwango cha kiambo (APELL) Kitabu cha maelekezo. Lililozinduliwa mwaka wa 2015, toleo hili jipya linabaibainisha umuhimu wa mbinu mbalimbali jumuishi za hatari katika ngazi za kiambo, na husisitiza umuhimu wa washikadau wengi na wahusika wote wa jamii. 

Pia, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Hatari ya Maafaa katika ripoti ya mwaka wa 2018 ilieleza athari kubwa ya kifedha ya maafa yanayohusiana na hali ya hewa. Kulingana na ripoti, “miaka ishirini iliyopita kumekuwa na kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa asilimia 151 katika hasara ya moja kwa moja ya kiuchumi kutokana na maafa yanayohusiana na hali ya hewa”.

Mami Mizutori, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Kupunguza Hatari ya Maafa ameingia kwenye rekodi akisema: “Kimbunga Idai ni onyesho wazi la kuhatarishwa na mazingira magumu kwa jiji na miji mingi ya nyanda za chini kwa kupanda kwa kiwango cha bahari kama athari ya mabadiliko ya hali ya hewa yanaendelea kuathiri na kuharibu hali ya hewa ya kawaida.”

“Athari za mabadiliko ya hali ya hewa kama kimbunga Idai zitaonekana zaidi na zaidi tunapoendelea na athari zitakua zaidi; mabaya zaidi bado yatakuja, “Happison Chikova, mtaalam wa kujitegemea wa mabadiliko ya hali ya hewa nchini Zimbabwe, aliiambia IDN.

Hata kwa wataalamu wa metorolojia kama Chimango Simengwa wa Malawi “ongezeko la halijoto duniani kote pamoja na ongezeko la joto baharini, linasababisha kimbunga cha chemchela”. Halijoto za hewa yenye joto zinamaanisha mvua inashikiliwa juu na kisha kuachiliwa kupitia vimbunga kama vile Idai, anasema Joseph Tasosa wa Itibari ya Kimazingira ya Zimbabwe. “Kimbunga Idai kilikuja pamoja na mvua yenye thamani ya mwaka kwa muda mfupi,” Tasosa anaongeza.

Kinyume cha historia hii, wachunguzi wanakumbuka kwamba katika kikao cha kumi na saba cha Mkutano wa Wanachama (COP 17) cha Mkusanyiko wa mfumo wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) jijini Durban, mataifa tajiri duniani yaliahidi kutoa msaada wa dola za marekani bilioni 100 kwa mwaka katika misaada ya kurejesha hali ya hewa kwa mataifa masikini kufikia mwaka wa 2020. Hata hivyo, asilimia 10 tu ya fedha za mabadiliko ya hali ya hewa zimehifadhiwa hadi sasa. [IDN- InDepthNews – 01 Mei 2019]

Picha: Kimbunga Idai kimeathiri maisha na njia za kujipatia riziki za watu karibu milioni tatu nchini Msumbiji, Zimbabwe na Malawi. Imeandaliwa na: UNDP Zimbabwe

NEWSLETTER

STRIVING

MAPTING

PARTNERS

Scroll to Top