Home – SDGs for All

A project of the Non-profit International Press Syndicate Group with IDN as the Flagship Agency in partnership with Soka Gakkai International in consultative status with ECOSOC

Watch out for our new project website https://sdgs-for-all.net

Mashindano ya Jamii ya Asili ya Tanzania Kulinda Ardhi Inayolengwa na Wawekezaji

Na Kizito Makoye

DAR ES SALAAM (IDN) – Helena Magafu alitabasamu alipopata hati ambayo inamtambua kama mmiliki pekee wa ardhi inayoshindaniwa katika kijiji chake ilipeanwa kwake, na hivyo kutatua mgogoro mkali na majirani zake.

“Nina furaha sana, sidhani mtu yeyote atadai tena kuwa ardhi hii ni yao,” alisema

Kwa miaka nane iliyopita mjane mwenye umri wa miaka 53, ambaye anaishi katika kijiji cha Sanje katika wilaya ya vijijini ya Kilombero – katika Mkoa wa Morogoro, kusini-magharibi mwa Tanzania – amekuwa akiwa na mgogoro na majirani zake ambao walijaribu kuchukua hekta 30 za ardhi ya familia yake wakati mumewe alikufa.

Read More...

Afrika Imejitolea Kwa Usawa Wa Kijinsia, Uwezeshaji Wa Wanawake

Na Jeffrey Moyo

JOHANNESBURG (IDN) – Ruramai Gwata mwenye umri wa miaka ishirini na tisa hakuwa na sababu ya kusherehekea Siku ya Wanawake ya Kimataifa inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka. Alilala hospitali akiuguza majeraha yake baada ya kushambuliwa vibaya na mume wake juu ya mgogoro wa nyumbani.

Alipokuwa akipambana na maumivu yake miezi miwili baadaye, dunia ilipokuwa ikikumbuka Siku ya Mama, Gwata alikuwa na shida ya kumbukumbu za maumivu jinsi watoto wake wawili walivyoona kunyanyaswa kwake na mumewe.

Read More...

Upatikanaji wa Teknolojia za Matumizi ya Mwisho Umuhimu wa Kuboresha Maendeleo katika Afrika

Na Joshua Masinde

NAIROBI (IDN) – Matumizi ya nishati kwa ufanisi yana ufunguo wa mabadiliko ya maisha vijijini mwa Afrika. Makampuni madogo yanaweza kuboresha taratibu zao za uzalishaji na ufanisi kama yangepata ufanisi bora wa umeme na teknolojia.

Bila umeme, biashara ndogo za vijijini hutumia zana ambazo sio za kisasa za mwongozo wenye nguvu za kibinadamu na za kupoteza muda, na mara nyingi hugeuka fursa nyingi za kuongeza thamani au bidhaa mbalimbali.

Kuridhisha haja ya nguvu za umeme za makampuni ya kibiashara hutoa fursa kwa wahusika wa sekta ya kibinafsi kama JUMEME, kampuni ya Tanzania inayoendeleza mini-gridi (nishati) za jua ili kuunganisha biashara na kaya katika maeneo ya mbali.

Read More...
Photo: Members of the women's cooperative use climate-resilient organic compost and biopesticides in their farm. Credit: UN Women

Wanawake Wakulima wa Afrika Wanapambana na Athari ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa

Na Ronald Joshua

NEW YORK | BAMAKO (IDN) – Fatou Dembele ni mkulima katika nchi ya Mali isiyo na bandari, ambapo nusu ya wakazi wanaohusika katika kilimo ni wanawake. Kilimo ni sekta muhimu ya kuinua wanawake kutokana na umasikini. Lakini uharibifu unaoongezeka wa ardhi na rasilimali za asili unaosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa unawafanya wanawake wawe katika hatari zaidi.

Kwa hivyo wakati mimea ya Dembele ilianza kufa, alifikiri shamba hilo liliharibiwa, na maisha yake yalikuwa katika hatari. “Tulifikiri shamba lilikuwa na ugonjwa. Hatukujua ya kwamba kulikuwa na vimelea vya kuishi vilivyoshambulia mizizi ya mimea na kuweza kuiua,” anasema Dembele.

Read More...

Tanzania Inashinikiza Uwezeshaji Wa Kijinsia Licha Ya Vikwazo

Na Kizito Makoye

DAR ES SALAAM (IDN) – Licha ya jitihada za kukuza usawa wa kijnsia, wanawake na wasichana nchini Tanzania bado wamepuuzwa na kwa kiasi kikubwa wananchi wasiotumika – mara nyingi wanakabiliwa na ubaguzi na unyanyasaji kutoka kwa wenzao waume kwa sababu ya mfumo wa usimamiaji wa upendeleo wa wanaume ambao mara kwa mara unasukuma wanawake kwa ukingo wa kuishi.

Hata hivyo, kulingana na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), mipango mbalimbali inatekelezwa ili kuwawezesha wanawake, ingawa bado wanakabiliwa na vikwazo vinavyowazuia kufikia uwezo wao kamili.

Read More...

Yatima wa Migogoro nchini DR Congo Wanajifunza Sanaa ya Kibrazili ya Kuondokana na Maumivu

 Na Fabíola Ortiz 

GOMA (IDN) – Tangu Februari mwaka huu, Melvin * mwenye umri wa miaka 16 anaishi katika makazi ya askari watoto wa zamani katika vitongoji vya Goma, mji mkuu wa jimbo la Kaskazini Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Yeye ni wa jamii ndogo. 

Hadithi yake inafanana na ya wavulana wengi wa Kongo wanaoishi katika jamii za mbali mashariki mwa DRC. Alikamatwa kutoka kijiji chake cha nyumbani ili kujiunga na waasi wa Nyatura – kikundi cha silaha kilichoongozwa na jamii ya Mayi-Mayi kilichoanzishwa mwaka 2010 hasa na Wahutu wa Kongo. Miongoni mwa ukiukwaji wa haki za binadamu walioshutumiwa ni kuajiri askari watoto – mojawapo ya makosa mabaya zaidi waliyoyatenda. 

Read More...

Kufanya Mwongo wa Tatu wa Maendeleo ya Viwanda Afrika kuwa Uhakika kwa Vitendo Mashinani

Na J Nastranis

UNITED NATIONS (IDN) – Wakati Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipitisha Azimio kutangaza 2016-2025 kama Mwongo waTatu wa Maendeleo ya Viwanda ya Afrika (IDDA III) miaka miwili iliyopita, ilisema: “Afrika bado ni kanda maskini sana na yenye hatari zaidi. Duniani.” Na hii licha ya miongo miwili iliyopita.

Azimio la A / RES / 70/293 lilibainisha “haja ya bara kufanya hatua za haraka ili kuendeleza viwanda vilivyo endelevu kama kipengele muhimu cha kuendeleza uwiano wa kiuchumi na kuongeza thamani, kuunda ajira na hivyo kupunguza umasikini,” na kuchangia utekelezaji wa Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu.

Read More...
Najma Hassan cooking in her kitchen in Kakuma refugee camp, Kenya, Credit: Justus Wanzala | IDN-INPS

Nishati safi Yaja Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma Kenya

Na Justus Wanzala

KAKUMA, Kenya (IDN) – Wakati jua linapoingia kwenye mpira nyekundu kutoweka kwenye upeo wa macho, wakazi wa kambi ya wakimbizi ya Kakuma katika Kata ya Turkana, kaskazini-magharibi mwa Kenya, hujirekebisha kwa mambo yale yale ya jioni. Wafanyabiashara wa kuchelewa wanakimbilia maduka ya chakula, watoto wa shule wanachukua vitabu vyao na wamama wanaanza kuandaa chakula cha mwisho cha siku.

Giza inakuza haraka kambi – ambayo inasimamiwa na Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (UNHCR) – na ni biashara na makazi machahe tu yaliyo na nafasi nzuri ya kuwa na jenereta za dizeli au taa za jua na mafuta ya taa ili kutoa mwangaza.

Read More...

Kwa nini kutumia dollar thelathini kwa mwaka kwa kila kijana ni muhimu

Imeandikwa na J Nastranis

NEW YORK (IDN) – Kulingana na utafiti wa tume ya UNFPA, United Nations Population Fund, utumizi wa chini ya dola thelathini kwa kila mtu kwa kila mwaka unaweza kufanya maajabu kwa afya na elimu ya vijana .

Ripoti imechapishwa kwa Lanceti siku moja kabla ya mikutano ya World Bank Spring mjini Washington D.C.kuanzia mwezi wa Aprili 21 hadi Aprili 23, 2017, ambapo viongozi wa kifedha na maendeleo kutoka nchi 188 wamepangiwa kuchangia umuhimu wa kuwekezea vijana .

Read More...

NEWSLETTER

STRIVING

MAPTING

MAPTING

Scroll to Top