Home – SDGs for All

A project of the Non-profit International Press Syndicate Group with IDN as the Flagship Agency in partnership with Soka Gakkai International in consultative status with ECOSOC

Watch out for our new project website https://sdgs-for-all.net

Ajenda Ya Maendeleo Mapya Ya Umoja Wa Mataifa Inateua Wajibu Mpya kwa Vijana

Na Rodney Reynolds

UMOJA WA MATAIFA (IDN) – Katibu Mkuu Ban Ki-moon, ambaye ameendelea kusisitiza jukumu muhimu kushughulikiwa na vijana katika utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo (MEM) ya 17 ya Umoja wa Mataifa ifikapo mwaka wa 2030, anasema kuwa vijana wengi duniani kote wamekuwa wakiathiriwa na migogoro ya kiuchumu na kushuka kwa uchumi.

“Kama viongozi wa tochi wa ajenda ya maendeleo mapya, mna jukumu muhimu kushughulikia katika kukomesha umaskini, kukosekana kwa usawa, njaa na uharibifu wa mazingira. Hatua zenu zitakuwa katikati katika kukaribisha kipindi ambapo hakuna mtu anaachwa nyuma,” aliambia mkutano wa vijana.

Read More...

Baraza la Usalama Lilitoa habari juu ya Migogoro Inayosababisha Njaa Kali

Uchambuzi na Jaya Ramachandran

BERLIN | ROMA (IDN) – Barasa la Usalama wa Umoja wa Mataifa linakabiliwa na changamoto kama si hali isiyo ya kawaida: imeonywa kuwa “migogoro ya muda mrefu inayoathiri nchi 17” sasa imeingiza zaidi ya watu milioni 56 ndani ya viwango vya aidha “matatizo” au “dharura” ya uhaba wa chakula na inazuia jitihada za kimataifa za kukomesha utapiamlo.

Wakati huo huo, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira na Taasisi ya Rasilimali za Dunia (TRD), kuhusu theluthi moja ya chakula chote kinachozalishwa duniani kote, chenye thamani ya karibu dola trilioni 1 za Marekani, zinapotea au kuharibiwa katika mifumo ya uzalishaji wa chakula na matumizi.

Read More...

Zimbabwe Inapigania Kukuza Kukua kwa Uchumi Endelevu

Uchambuzi na Jeffrey Moyo

HARARE (IDN) – Sawa katika suruali zilizofifia na shati na jozi mzee ya viatu yenye madoa ya mchanganyiko wa viraka na mashimo, Jemitius Simango mwenye umri wa miaka 38 hutembea kando ya Barabara ya Kwanza katika mji mkuu wa Zimbabwe na gunia kubwa lenye chupa tupu za plastiki mgongoni mwake akifukua mapipa ya takataka katika kutafuta thamani.

Simango ana Stashahada ya Masoko kutoka Chuo cha Ufundi cha Harare nchini Zimbabwe na katika mtazamo wa kwanza wengi humuona kama kichaa, ingawa yeye ni mtu wa kawaida katika ‘kazi’ akijaribu kuendesha maisha dhidi ya kuongezeka kwa uchumi wa kushindwa katika hili taifa la Kusini mwa Afrika. Baada ya kushindwa kupata ajira, wengi kama Simango wamegeuka kufanya kazi duni mbalimbali kwa maisha yao.

Read More...

Waafrika Wanaapa Kukuza ujenzi wa Viwanda wenye Ushirikiano na Uendelevu

Uchambuzi na Jeffrey Moyo

HARARE (IDN) – Jukwaa la tatu la Maendeleo lenye Uwezo wa Kiafrika lililoandaliwa na Msingi wa Ujenzi wa Uwezo wa Kiafrika (MUUK), kwa ushirikiano na wadau wa shirika la Kiafrika na washirika wa kimataifa, wameapa kuboresha sekta ya viwanda pamoja na miundombinu, ili kukuza ujenzi wa viwanda wenye ushirikiano na uendelevu na kuendeleza ubunifu katika njia moja na lengo la tisa la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Kimataifa.

Read More...

Zimbabwe Inafanya Mafanikio katika Kufikia Usawa wa Kijinsia

Uchambuzi na Jeffrey Moyo

HARARE (IDN) – Pamoja na vikwazo wanawake wanaendelea kukabiliana navyo nchini Zimbabwe, nchi hii imefanya mafanikio makubwa katika kufikia usawa wa kijinsia katika msitari na Lengo la 5 la Malengo Endelevu ya Maendeleo (MEM) yanayotazamiwa kupatikana ifikapo mwaka 2030.

Kuna uwakilishi bora wa wanawake bungeni na kuongezeka kwa idadi ya wasichana katika chuo kikuu kuliko wenzao wa kiume kwa sasa  – na hii wanawake zaidi pia wamechukua kazi zinazoshikiliwa na wanaume.

Read More...

NEWSLETTER

STRIVING

MAPTING

MAPTING

Scroll to Top