Home – SDGs for All

A project of the Non-profit International Press Syndicate Group with IDN as the Flagship Agency in partnership with Soka Gakkai International in consultative status with ECOSOC

Watch out for our new project website https://sdgs-for-all.net

Ukuta Mkubwa wa Kijani (Great Green Wall) Unaandaa Njia ya Kufikia 2030

share
tweet
pin it
share
share

Na Rita Joshi

BONN (IDN) – Mpango wa Ukuta Mkubwa wa Kijani (GGW) kwa zaidi ya karibu miaka 13 umerejesha karibu hekta milioni 20 za ardhi, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Septemba tarehe 7 katika mkutano usio bayana wa mawaziri wa mazingira kutoka Senegali, Mauritania, Mali, Bukina Faso, Naija, Naijeria, Chadi, Sudani, Eritrea, Uhabeshi na Jibuti pamoja na washirika wa kikanda, mashirika ya kimataifa na mashirika ya maendeleo.

Mpango wa GGW ulizinduliwa mnamo mwaka wa 2007 chini ya uongozi wa Tume ya Umoja wa Afrika na Shirika la Muungano wa Afrika, na kwa msaada wa kifedha kutoka kwa serikali ya Ayalandi.

Mpango huo unaunganisha nchi za Kiafrika na washirika wa kimataifa kubadilisha maisha ya mamilioni ya watu kwa upanzi wa urefu wa kilomita 8,000 na upana wa kilomita 15 za miti, nyasi, majani na mimea kando ya ncha ya kusini mwa jangwa la Sahara. Mara tu ukikamilika, GGW itakuwa muundo mkubwa zaidi wa kuishi kwenye sayari, saizi mara tatu ya Great Barrier Reef.

Iliyopewa jina Great Green Wall: Hali ya Utekelezaji na Njia ya Kufikia 2030, ripoti hiyo ni ushuhuda wa hali wa kwanza kamili. Inasema kwamba zaidi ya ajira 350,000 zilipatikana na karibu dola milioni 90 katika mapato zilitengenezwa kutoka mwaka wa 2007 hadi 2018 kupitia shughuli za GGW.  

Zaidi ya watu 220,000 walipata mafunzo juu ya uzalishaji endelevu wa mazao ya kilimo cha mimea na ufugaji na yasiyo ya mbao kusaidia mabadiliko ya matumizi na uzalishaji unaowajibika zaidi. Eneo lililorejeshwa litatenga zaidi ya 300 MtCO2 ifikapo mwaka wa 2030, takriban asilimia 30 ya lengo linalotarajiwa la GGW.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kwamba kufikia urejeshwaji unaolengwa wa hekta milioni 100 za ardhi ifikapo mwaka wa 2030, nchi za GGW zinahitaji kurejesha hekta milioni 8.2 za ardhi kila mwaka katika uwekezaji wa kifedha wa kila mwaka wa dola bilioni 4.3. Mpango huo pia unalenga kuleta ajira milioni 10 kufikia tarehe hiyo. 

“Great Green Wall inaweza – na – itabadilisha ukweli ulioishi wa mamilioni ya watu wetu. Ajira zaidi, afya bora, uthabiti zaidi. Jamii zenye ustahimilifu na mshikamano na ukuaji thabiti wa uchumi unaojumuisha,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa- Bi. Amina Mohammed katika hotuba yake ya ufunguzi kwa mkutano wa mawaziri.

“Tunapochunguza mabaki ya COVID-19 na kufanya mipango yetu ya kujenga upya kupitia vifurushi imara vyenye kichocheo, itakuwa fursa iliyokosekana kutokuona kuwekeza kwenye Great Green Wall kama sehemu muhimu ya mwitikio na urejesho endelevu wa uchumi wa pamoja,” Bi Mohammed aliongeza.

Katibu Mtendaji wa UNCCD Bwana Ibrahim Thiaw pia alisisitiza:  “GGW inatoa faida za haraka kwa jamii za kiambo na faida za viumbe hai kwa muda mrefu katika kiwango cha kimataifa. Inaonyesha kuwa wakati nchi zinathubutu kuota, kufanya kazi pamoja na kufanya uamuzi sahihi, tunaweza kufanikiwa na kuishi kwa amani na maumbile. Na pale mawazo ya ubunifu yanaibuka, mabadiliko mazuri, makubwa yanayonufaisha jamii za kiambo na za kimataifa yatatokea.”

Wakati wa kufunga mkutano wa mawaziri, tamko juu ya Great Green Wall lilipitishwa kuonyesha uwezo wa GGW kama moja ya hatua za kufikia kufufua uchumi baada ya COVID, kupunguza umaskini, urejesho wa viumbe hai, kuzoea na kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa, kuwawezesha wanawake, vita dhidi ya uhamiaji wa kiuchumi usio wa kawaida na upatikanaji wa ajira.

Tamko hilo linasisitiza hitaji la msaada endelevu na anuwai na pia ushiriki halisi wa washirika wote kufikia malengo ya GGW.

Mawaziri, wawakilishi wa mataifa wanachama wa Shirika la Muungano wa Afrika wa Great Green Wall wa Bukina Faso, Jibuti, Eritrea, Uhabeshi, Mali, Mauritania, Naija, Naijeria, Senegali, Sudani na Chadi walionyesha wasiwasi mkubwa kuhusu “hali ya sasa ya afya duniani kutokana na janga la COVID-19, ambalo matokeo yake ya kijamii na kiuchumi katika muda mfupi, wa kati na mrefu pia yatakuwa na athari fulani kiikolojia “.

Dhidi ya kinyume hiki, kuanzisha amani na utulivu wa kudumu katika eneo la Sahel kunahitaji jitihada za pamoja katika maeneo ya usalama, maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa kijamii;

Katika tamko lao, Mawaziri walisisitiza kwamba utekelezaji wa Mpango wa Great Green Wall ni/na unabaki kipaumbele kwa kila moja ya nchi zetu wanachama kumi na moja. Tunarudia maono yetu ya pamoja ya kufanya Great Green Wall kuwa moja ya hatua za kufanikisha kufufua uchumi baada ya COVID, kufanikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, Ajenda ya 2063 na Mkataba wa Paris katika nchi zetu.

Waliwataka washirika wote kutoa msaada endelevu na anuwai kwa nchi wanachama wa Shirika la Muungano wa Afrika kwa Great Green Wall, kwani utekelezaji wa Great Green Wall ni kipaumbele kwa Mataifa yetu, ambao unaweza kuchangia katika kupatikana kwa ajira, utajiri na mafanikio.

Waliwahimiza washirika wa maendeleo kuunganisha juhudi zao na mipango ili kuchangia, na kuwezesha, mipangilio ya kuingilia yenye lengo, miongoni mwa mengine, katika kupunguza umaskini, urejesho wa viumbe hai, kuzoea, na/au, kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa, kuwawezesha wanawake, vita dhidi ya uhamiaji wa kiuchumi usio wa kawaida na upatikanaji wa ajira katika maeneo ya vijijini.

Waliwataka zaidi washirika wao, hasa Green Climate Fund, Mkusanyiko wa Umoja wa Mataifa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa, Tawi la Mazingira ya Kimataifa, Kikundi cha Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Kikundi cha Benki ya Maendeleo ya Afrika na pia Shirika la Maendeleo ya Kifaransa na washirika wengine wa pande mbili wanaovutiwa, kusaidia Mataifa yetu katika kuendeleza mpango wa mwavuli kwenye Great Green Wall. [IDN-InDepthNews – 16 Septemba 2020].

Picha- hisani: UNCCDC

NEWSLETTER

STRIVING

MAPTING

PARTNERS

Scroll to Top