Serikali za Kiafrika Zinajiunga na Wanaharakati Kupambana na Ulipizaji/Ufisadi wa Kingono
Na Kizito Makoye
DAR ES SALAAM (IDN) – Bango lenye ujumbe “Hitimu na ‘A’ sio na UKIMWI” katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, linaeleza hadithi mbaya ya wanafunzi wa kike ambao hushiriki ngono ili kupata alama za juu.
“Mwalimu wangu alitaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mimi. Nilipokataa matakwa yake ya ngono, alilipiza kisasi kwa kunipa alama za chini,” anasema Helena (si jina lake halisi).
Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 anayesomea sheria, ambaye amepitia utendaji duni katika masomo yake, anazidi kuwa na wasiwasi kuhusu hatma yake ya kitaaluma.…