NOTE! This site uses cookies and similar technologies.

If you not change browser settings, you agree to it.

I understand

Reporting the underreported about the plan of action for People, Planet and Prosperity, and efforts to make the promise of the SDGs a reality.
A project of the Non-profit International Press Syndicate Group with IDN as the Flagship Agency in partnership with Soka Gakkai International in consultative status with ECOSOC.


SGI Soka Gakkai International

 

Serikali za Kiafrika Zinajiunga na Wanaharakati Kupambana na Ulipizaji/Ufisadi wa Kingono

Na Kizito Makoye

DAR ES SALAAM (IDN) – Bango lenye ujumbe "Hitimu na ‘A’ sio na UKIMWI" katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, linaeleza hadithi mbaya ya wanafunzi wa kike ambao hushiriki ngono ili kupata alama za juu.

"Mwalimu wangu alitaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mimi. Nilipokataa matakwa yake ya ngono, alilipiza kisasi kwa kunipa alama za chini," anasema Helena (si jina lake halisi).

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 anayesomea sheria, ambaye amepitia utendaji duni katika masomo yake, anazidi kuwa na wasiwasi kuhusu hatma yake ya kitaaluma.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kinachojulikana kwa utendaji bora wa kitaaluma, kilikuwa katika uangalizi mwishoni mwa mwaka wa 2018 baada ya madai ya ulipizaji wa kingono dhidi ya wanafunzi wa kike.

Akiwa ameketi chini ya mti mkubwa mbuyu ambapo marafiki wanakusanyika kwa majadiliano ya kikundi, Helena, ambaye ni mmoja tu wa wanafunzi wengi ambao wamekuwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono, amevunja ukimya wake.

"Nimetoa ripoti ya suala hilo kwa mamlaka ya kupambana na ufisadi, natumaini watanisaidia," anasema.

Tamaduni ya aibu inayomeza jamii ya chuo kikuu imefanya kuwa vigumu zaidi kwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono kuelezea hadithi zao, kulingana na vikundi vya haki za wanawake.

Kama sehemu ya jitihada zake za kuzuia unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake, Ofisi ya Shirika la Kuzuia na Kupambana na Ufisadi la Tanzania (PCCB), imeanzisha madawati ya kijinsia, ambapo waathirika wa kingono wanaweza kufungua kesi zao na maafisa wa kike.

Ulipizaji wa kingono ni aina ya rushwa ambapo watu wenye vyeo vya mamlaka hulipiza ngono kutoka kwa wanafunzi au wanawake wanaotafuta kazi au kupandishwa vyeo kwa kutumia msisitizo wa maneno.

Hatua ya kuanzisha madawati ya kijinsia, ambayo yanakuja miaka miwili baada ya nchi ya Afrika Mashariki kupitisha miongozo ya kimaadili, kwa minajili ya kuzuia tabia mbaya miongoni mwa watumishi wa umma, inasifiwa kama hatua kubwa katika mapambano dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, wanasema wanaharakati wa haki za wanawake.

Ulipizaji wa kingono ni tukio la kimataifa ambapo ufisadi na unyanyasaji wa kijinsia hupitana. Ingawa tatizo hilo husababisha dhiki ya kimwili na kiakili kwa waathirika, mamlaka yameshindwa mara nyingi kulishughulikia.

Diwani Athumani, Mkurugenzi Mkuu wa PCCB, alieleza kwamba mpango wa ofisi umekusudia kutafuta haki kwa waathirika wa ulipizaji wa kingono, kwa lengo la kukomesha unyanyasaji wa kijinsia katika mfumo uliokithiri wa wanaume.

"Tunahimiza wanawake kujitokeza na kuongea dhidi ya rushwa ya ngono," alisema. "Kuvunja ukimya wao kutawasaidia kuwa upande unaostahili wa sheria."

Kwa mujibu wa Athumani, ofisi pia imezindua simu ya bure ya watu kuripoti unyanyasaji wa kingono.

Wakati ulipizaji wa kingono ni kosa la jinai nchini Tanzania, wanaharakati wanasema sheria ni dhaifu mno kuzuia wahusika ambao mara nyingi hulipa faini na kuachiliwa huru.

Sehemu ya 25 ya sheria ya kupambana na ufisadi ya Tanzania ya mwaka wa 2007 inasema hivi: "Mtu yeyote akiwa katika wadhifa wa mamlaka, ambaye katika shughuli za mamlaka yake, anadai au anatoa vibali vya kingono, au vibali vingine vyovyote kwa mtu yeyote kama hali ya kutoa ajira, kupandisha cheo, haki, upendeleo, au maonevu mengine yoyote, anafanya kosa na atawajibika, kwa kuhukumiwa, kwa faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo cha muda usiozidi miaka mitatu au zote mbili."

Kupigania haki ya kijamii ni sehemu ya mfumo unaokua barani Afrika, ambapo serikali zimeungana na wanaharakati wa haki za wanawake ili kukabiliana na wimbi linalopanda la unyanyasaji wa kijinsia.

Kutoka Kigali hadi Accra, kutoka Nairobi hadi Lagos, mamlaka na wanaharakati wa haki za wanawake wanathibitisha ustadi katika kujenga vitengo vya umma vya kirafiki kujadili hali isiyofaa ya unyanyasaji wa kijinsia.

Nchini Rwanda, serikali ilianzisha dawati la kijinsia mwaka wa 2005 ikisaidiwa na Wanawake wa Umoja wa Mataifa, kuimarisha ulinzi wa wanawake kutokana na unyanyasaji.

Wakati sheria za kupambana na ufisadi zinatoa sababu za kushtaki ulipizaji wa kingono, wachambuzi wanasema kuwa sharia za ubaguzi wa kijinsia na za unyanyasaji mara nyingi hulenga aina ya unyanyasaji uliohusishwa katika ulipizaji wa kingono.

"Meneja anayefanya ukiukwaji wa mamlaka yake kwa kulipiza ngono kutoka kwa afisa wa ngazi ya chini anayetaka kuepuka kupigwa kalamu, anajishughulisha katika zote mbili; unyanyasaji wa kingono kwa faida fulani na ulipizaji wa kingono," alisema Eliana Mbugua, mtaalamu wa haki za kijinsia kutoka nchini Kenya.

Kulingana na Mbugua, sheria nyingi za unyanyasaji wa kingono zimefungwa kwa ajira na zinahusisha tu vikwazo vya utawala.

Nchini Tanzania, ambapo karibu tisa katika kila wanawake 10 wamepitia unyanyasaji wa kingono, wanaharakati wanasema kuwa na madawati ya kijinsia ambapo waathirika wa unyanyasaji wa kingono wanaweza kuelezea hadithi zao kwa maafisa walio na mafunzo ni hoja nzuri.

Leila Sheikh, mwanaharakati wa haki za kijamii aliye huko Dar es Salaam, aliyepitia unyanyasaji wa kingono wakati alikuwa akifanyia kazi Tume ya Tanzania ya UKIMWI zaidi ya miaka kumi iliyopita, anawahimiza wanawake kupaza sauti zao dhidi ya uovu.

"Wanawake wanapaswa kuzungumza, kupaza sauti zetu dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia. Akizungumza anaweka gurudumu la haki katika mwendo," anasema.

Ulipizaji wa kingono, ambao huathiri kujiamini, ni vigumu kuthibitisha kwa vile unafanyika kwa siri na ushahidi haupatikani. Wakati ushahidi usioaminika unaonyesha kuenea kwa tatizo, mamlaka hayajaweka rekodi ya data awali kutokana na unyanyapaa na aibu.

Katika chombo cha zana cha mwaka wa 2012 kiitwacho "Kutaja, Kuaibisha na Kumaliza Ulipizaji wa kingono", Shirikisho la Kimataifa la Wanawake Majaji lilionyesha mapengo katika mifumo ya haki ya makosa ya jinai duniani kote katika kujadili ulipizaji wa kingono, huku likipendekeza hatua za kuboresha sheria na sera za kinyumbani.

Chris Peter Maina, Profesa wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anapinga ulipizaji wa kingono kwa misingi kwamba unakiuka maadili ya kimsingi, na kuwataka watu wenye vyeo vya mamlaka kuacha kunyanyasa kingono watu wa vyeo vya chini ambao wanawaongoza.

"Ingawa kutongoza mtu hakuanzishi ukiukaji wa sheria, watu wenye mamlaka hawapaswi kutumia mamlaka yao vibaya," alisisitiza.

Maina anawahimiza waathirika wa ulipizaji wa kingono kujitokeza na kuwafichua wahalifu, akisema kwamba, hofu ya "waathirika’ kufichua wahalifu ni kikwazo kikubwa cha kupambana kwa ufanisi dhidi ya ulipizaji wa kingono." [IDN-InDepthNews – 12 Juni 2019]

Picha: Wanawake wanashiriki katika maandamano kupinga ulipizaji wa kingono huko Dar es Salaam mwaka wa 2018. Hisani: Edwin Mjwahuzi

Newsletter

Striving

Striving for People Planet and Peace 2022

Mapting

MAPTING

Partners

SDG Media Compact


Please publish modules in offcanvas position.